(Picha : Xinhua)

Rais wa China Xi Jinping, akiongoza ujumbe mkuu, aliwasili Lhasa, mji mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Xizang, Jumatano kuhudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya kuanzishwa kwa eneo hilo.

Xi Jinping, pia katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Tume Kuu ya Kijeshi, na ujumbe aliouongoza walipata mapokezi makubwa kutoka kwa watu wa makabila mbalimbali huko Xizang, katika uwanja wa ndege na katika mji wa Lhasa.

Xi Jinping ameandamana na Wang Huning, mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Watu wa China (CPPCC) na mkuu wa ujumbe mkuu, na Cai Qi, mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kamati Kuu ya CPC. Wang Huning na Cai Qi wote ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Kisiasa ya Kamati Kuu ya CPC.